Kuanzishwa kwa Huduma ya Bezaleli

Tumeamua kuanzisha huduma hii ya kujenga na kuongeza thamani, kupitia ukarabati, wa makanisa ya SDA hapa Tanzania na popote Mungu atakapotuita. Tunaamini Mungu alikuwa na kusudi nasi katika harakati hii alipotuongoza katika ufadhili, usanifu ujenzi, ukarabati, usimamizi ujenzi na katika kutoa misaada mbali mbali (Suguti, Mbaga, Chalinze, Makongo, Nyamato, nk.) ili kuongeza nafasi za waabudu makanisani, kusogeza huduma kwa wanaotafuta kumjua Mungu katika ibada, kuonyesha kipaumbele cha mkiristo katika shughuli zake za imani, hususani kutoa kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za ibada.


Huduma hii tunaipa jina la BEZALELI (Kutoka 31:2-11 na 36:1- 3), mtumishi wa Mungu katika ujenzi wa hema la kukutanikia (Kutoka 25-31; 36-40). Itafanya kazi kwa kupokea matoleo ya kila mtu ambaye “moyo wake wampa kupenda” sawasawa na neno la Mungu kwamba: “Waambie wana wa Israel kwamba wanitwalie sadaka; kila mtu ambaye moyo wake wampa kupenda mtatwaa kwake sadaka yangu (Kutoka 25: 2)”. Na watatenda kazi hii kama alivyoagiza Mungu: “Basi Bezaleli na Oholiabu watatenda kazi na kila mtu mwenye moyo wa hekima, ambaye BWANA amemtia akili na hekima, ili ajue kufanya kazi hiyo yote kwa huo utumishi wa mahali patakatifu, kama hayo yote BWANA aliyoyaagiza (Kutoka 36:1)”.


Wito Wetu

Angalia nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa uri, mwana wa Huri wa kabila ya Yuda; nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mabo ya kazi ya kila aina, ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba, na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya usitadi iwayo yote (Kutoka 31: 2-5). 

Kwa wito kama huu Bazaleli inaanzishwa chini ya uongozi wangu Furaha Ngeregere Lugoe, Ph.D. na ushiriki wa karibu sana wa mke wangu, Grace na watoto wetu.

… Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa katikati yao. Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya (Kutoka 25:8, 9).

 Uzoefu wetu katika mtaa wa Suguti, ukiongozwa na mchungaji Ezekiel Zenge, unaonesha kuwa makanisa mazuri yanavuta watu kwa Yesu na inabidi makanisa yawepo kila mahali palipo na kundi.

          

Hili ni hitaji la msingi sana. Hatuna takwimu bado ya kuonesha hitaji halisi sasa lakini kwa kuhesabu makundi wote tunaweza kusema ya kwamba hitaji ni kubwa sana. Pia jengo la kanisa liwe zuri si bora kanisa, na viti vyake viendane na uzuri wa jengo. Palipo na wawili au watatu Mimi nipo katikati yao asema BWANA. Tumkaribishe wapi?

Basi mkutano wote wa wana wa Israel wakaondoka hapo mbele za Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu (Kutoka 35:20, 21).


Ungana Nasi