Familia Ya Dkt. Furaha Lugoe

 

Familia yangu imejihusisha na ujenzi wa makanisa kwa takribani miaka 15 sasa ndani na nje ya huduma rasmi ya kanisa.

Kuanzishwa kwa Huduma ya Bezaleli

Tumeamua kuanzisha huduma hii ya kujenga na kuongeza thamani, kupitia ukarabati, wa makanisa ya SDA hapa Tanzania na popote Mungu atakapotuita.

Mungu atakapotuita. Tunaamini Mungu alikuwa na kusudi nasi katika harakati hii alipotuongoza katika ufadhili, usanifu ujenzi, ukarabati, usimamizi ujenzi na katika kutoa misaada mbali mbali (Suguti, Mbaga, Chalinze, Makongo, Nyamato, nk.)

 ili kuongeza nafasi za waabudu makanisani, kusogeza huduma kwa wanaotafuta kumjua Mungu katika ibada.

Soma Zaidi

Bezaleli kujenga Makanisa

Familia yangu imejihusisha na ujenzi wa makanisa kwa takribani miaka 15 sasa ndani na nje ya huduma rasmi ya kanisa. Kuanzia mwaka 2011/12 tumeona vyema kumfanyia BWANA kazi kwa kutumia fedha na uzoefu wetu kukarabati, kukamilisha na kujenga makanisa. 

Katika hili tumeuona mkono wa BWANA ukifanya kazi nasi na kugundua udhaifu mkubwa uliopo katika ujenzi na ukarabati wa makanisa yetu. Tunadhani tunaweza kwa kiasi Fulani kusaidia kurekebisha hali hii kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 

Soma Zaidi