Kujenga Makanisa Mapya

Uzoefu wetu katika mtaa wa Suguti, ukiongozwa na mchungaji Ezekiel Zenge, unaonesha kuwa makanisa mazuri yanavuta watu kwa Yesu na inabidi makanisa yawepo kila mahali palipo na kundi. Hili ni hitaji la msingi sana. Hatuna takwimu bado ya kuonesha hitaji halisi sasa lakini kwa kuhesabu makundi wote tunaweza kusema ya kwamba hitaji ni kubwa sana. Pia jengo la kanisa liwe zuri si bora kanisa, na viti vyake viendane na uzuri wa jengo. Palipo na wawili au watatu Mimi nipo katikati yao asema BWANA. Tumkaribishe wapi?

Biblia inasemaje juu ya hili?

… Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa katikati yao. Sawasawa na haya yote nikuoneshayo, mfano wa maskani, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyovifanya (Kutoka 25:8, 9).

Basi mkutano wote wa wana wa Israel wakaondoka hapo mbele za Musa. Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa BWANA, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu (Kutoka 35:20, 21).

Nao wakasema na Musa, na kumwambia, watu waleta vitu vingi sana zaidi zaidi ya hivyovitoshavyo kwa ajili ya utumishi wa hiyo kazi, ambayo BWANA aliiagiza ifanywe. Basi Musa akatoa amri, nao wakatangaza mbiu katika marago yote, wakisema, Wasifanye kazi tena, mtu mume wala mwanamke, kwa ajili ya matoleo kwa mahali patakatifu. Basi watu wakazuiwa wasilete tena. Kwani vile vitu walivyokuwa navyo vilikuwa vyatosha kwa kuifanya kazi hiyo yote kasha vilizidi (Kutoka 36:5-6). Kukarabati Makanisa

Makanisa yaliyo mengi yako katika hali ambayo ni mbaya hata waumini hawajisikii huru na amani kuketi hapo kama isingekuwa ni mazoea. Mengine yanajengwa kwa miaka mingi sana. BEZALELI Tungependa kuchangia katika kurekebisha hali hii katika kuhimiza washiriki na kutoa mkono wa fadhila penye haja hii. Tukumbuke sana alichofanya BWANA wakati wa nabii Hagai kwa waisraeli waliojali nyumba zao zaidi ya nyumba ya Mungu:

 “BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema BWANA (Hagai 1:7).

Mlitazamia vingi, kumbe vikatokea vichache, tena mlipovileta nyumbani nikavipeperusha. Ni kwa sababu gani? Asema BWANA wa majeshi. Ni kwa sababu ya nyumba yangu inayokaa katika hali ya kuharibika, wakati ambapo ninyi mnakimbilia  kila mtu nyumbani kwake. Basi kwa ajili yenu mbingu zimezuiliwa zisitoe umande, nayo nchi imezuiliwa isitoe matunda yake (Hagai 1:9-10).

Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi. Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi (Hagai 2:8, 9).

Hii ni sehemu ya pili na ya muhimu sana ya huduma ya BEZALELI. Tunadhani ya kwamba inawezekana sana wote tukijiwekea lengo la miaka mitano kuondokana na majengo ya miti, matofali ya tope au yaliyoezekwa kwa nyasi. Kwa Mungu wetu, yote haya yanawezekana.Kuhubiri Wakati wa Ujenzi

Huduma ya Bezaleli ni sehemu ya utume wa Yesu kwa wakristu sawasawa na Mathayo 28:19, 20 na kama utume huu unavyowekewa mkazo katika Ufunuo 10:11 kwa kanisa la masalia. 

Unasema, “ Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la baba, na mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari”. “Wakaniambia, imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi”.